Barcelona wapepeta Mallorca na kuendeleza presha kwa Real Madrid kileleni mwa jedwali la La Liga

Barcelona wapepeta Mallorca na kuendeleza presha kwa Real Madrid kileleni mwa jedwali la La Liga

Na MASHIRIKA

ROBERT Lewandowski alifungia Barcelona bao la pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Mallorca mnamo Jumamosi usiku na kuanika kiu ya kutamalaki Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) muhula huu.

Ni matokeo yaliyowezesha masogora hao wa kocha Xavi Hernandez kuendeleza presha kwa mabingwa watetezi Real Madrid ambao wamekuwa wakipishana nao kileleni mwa jedwali la La Liga.

Bao hilo la Lewandowski lilikuwa lake la tisa kutokana na mechi saba ambazo amesakatia Barcelona tangu abanduke kambini mwa Bayern Munich mwishoni mwa msimu jana.

Barcelona kwa sasa wanajivunia alama 19 baada ya kushinda mechi sita na kupiga sare moja kutokana na michuano saba iliyopita. Wafalme hao mara 26 wa La Liga wanajiandaa sasa kuvaana na Inter Milan katika gozi la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) hapo kesho ugani San Siro, Italia.

MATOKEO YA LA LIGA (Jumamosi):

Mallorca 0-1 Barcelona

Cadiz 0-0 Villarreal

Getafe 2-3 Valladolid

Sevilla 0-2 Atletico

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

WANTO WARUI: Waziri Machogu endapo ataidhinishwa asitarajie...

Wakulima wataka Ruto atimize ahadi ya mradi wa Bura

T L