Barcelona waponea kuondolewa na Granada kwenye Copa del Rey

Barcelona waponea kuondolewa na Granada kwenye Copa del Rey

Na MASHIRIKA

BARCELONA waliponea chupuchupu kubanduliwa kwenye Copa del Rey msimu huu baada ya kutatizwa na Granada ambao mwishowe walipokea kichapo cha mabao 5-3 mnamo Jumatano usiku ugani Nuevo de Los Carmenes.

Mabao ya muda wa ziada kutoka kwa Griezmann, Frenkie de Jong na Jordi Alba yaliwezesha Barcelona kusonga mbele na kutinga hatua ya nusu-fainali baada ya kutoka nyuma kwa mabao 2-0 katika dakika ya 88.

Magoli kutoka kwa Griezmann na Alba mwishoni mwa kipindi cha pili yalilazimisha mechi hiyo kuingia muda wa ziada baada ya Kenedy na Roberto Soldado kufungulia Granada ukurasa wa mabao awali.

Fede Vico alisawazishia Granada na kufanya mamabo kuwa 3-3 kupitia mkwaju wa penalti katika muda wa ziada.

Barcelona walielekeza makombora 36 langoni mwa wenyeji wao Granada na 20 kati ya mashuti hayo yakalenga shabaha.

Chini ya kocha Ronald Koeman, Barcelona kwa sasa wanaungana na Sevilla na Levante kwenye hatua ya nusu-fainali. Real Betis na Bilbao watakutana kwenye robo-fainali ya mwisho mnamo Februari 4, 2021.

Barcelona wanajivunia rekodi ya kufuzu kwa fainali ya Copa del Rey mara sita mfululizo kati ya 2014-2019 ambapo wametawazwa mabingwa mara nne katika kipindi hicho. Miamba hao wa soka ya Uhispania walidenguliwa na Athletic Bilbao kwenye hatua ya robo-fainali mnamo 2019-20.

TAFSIRI NA CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

‘Wazazi wetu walikuwa marafiki na ndio maana mimi na...

Mbappe na Di Maria wasaidia PSG kuendeleza presha kwa Lille