Michezo

Barcelona yamweka sokoni beki Samuel Umtiti

April 12th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

BARCELONA, Uhispania

KLABU ya Barcelona imemweka sokoni beki Samuel Umtiti.

Mfaransa huyo mshindi wa Kombe la Dunia amekuwa akihusishwa na Manchester United na sasa klabu yake imekubali kumuachilia kwa kitita cha kati ya Sh9 bilioni na Sh13 bilioni.

Huenda nafasi ya beki huyo aliyejiunga na Barcelona mnamo 2016 akitokea Lyon ikajazwa na Matthijs de Light wa Ajax Amsterdam ambaye bei yake imepanda siku hizi.