Barcelona yasajili vigogo Franck Kessie na Andreas Christensen bila ada yoyote

Barcelona yasajili vigogo Franck Kessie na Andreas Christensen bila ada yoyote

Na MASHIRIKA

BARCELONA wamesajili wanasoka Franck Kessie na Andreas Christensen bila ada yoyote.

Kessie ambaye ni raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 25, anatokea AC Milan ya Italia huku Christensen ambaye ni beki raia wa Denmark mwenye umri wa miaka 26 akitokea Chelsea.

Wawili hao wametia saini mkataba wa miaka minne kila mmoja na vikosi vitakavyowania maarifa yao baadaye vitalazimika kuweka mezani Sh63.6 bilioni ili kuwashawishi kuondoka ugani Camp Nou.

Kessie alichezea AC Milan mara 224 na akafunga jumla ya mabao 39. Mchango wake ulisaidia kikosi hicho kunyanyua Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa mara ya kwanza mnamo 2021-22 baada ya miaka 11.

Christensen alipokezwa malezi ya soka kambini mwa Chelsea ugani Stamford Bridge na akachezea The Blues mara 161 huku akitumwa kwa mkopo wa misimu miwili kambini mwa Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.

Anaondoka ugani Stamford Bridge akijivunia kushindia Chelsea taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), Europa League, Uefa Super Cup na Club World Cup.

Kiungo matata raia wa Brazil, Philippe Coutinho ameondoka rasmi ugani Camp Nou muhula na kujiunga na Aston Villa kwa mkataba wa kudumu uliogharimu Sh2.7 bilioni. Fowadi matata raia wa Ufaransa, Ousmane Dembele na beki wa kulia kutoka Brazil, Dani Alves wameagana na Barcelona baada ya kandarasi zao kutamatika.

Sogora mwingine anayetazamiwa kuondoka Barcelona ni kiungo mahiri raia wa Uholanzi, Frenkie de Jong, ambaye yuko pua na mdomo kuyoyomea Manchester United ya Uingereza kwa Sh8.3 bilioni.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Christian Eriksen akubali kujiunga na Man-United baada ya...

Montreal anayochezea Wanyama yaona cha mtema kuni dhidi ya...

T L