Barrow kutawala kwa muhula wa 2

Barrow kutawala kwa muhula wa 2

Na MASHIRIKA

RAIS Adama Barrow wa Gambia ameibuka mshindi kwa muhula wa pili, kulingana na matokeo ya uchaguzi uliofanyika nchini humo Jumapili.

Kulingana na tume kuu ya uchaguzi nchini humo, Barrow alizoa asilimia 53 ya kura. Mpinzani wake mkuu, Ousainou Darboel, alipata asilimia 27.7 ya kura.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Alieu Momarr Njai, alimtangaza Barrow kuwa mshindi saa chache baada ya wapinzani wake kukataa matokeo ya awali.

You can share this post!

Jeshi lamhukumu Suu Kyi miaka 4 gerezani

Matusi dhidi ya Raila yamwandama Uhuru

T L