NA KNA
JUHUDI za kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium kuhifadhi mazingira ya ardhi zilizotumiwa kwa shughuli za uchimbaji Kwale zimeshika kasi.
Msimamizi Mkuu wa masuala ya nje katika kampuni hiyo, Bw Simon Wall, alisema wamejitolea kuhakikisha ardhi zote zilitoathiriwa na uchimbaji madini zitarudishiwa rotuba zao, huku shughuli za uchimbaji zikitarajiwa kukamilika Novemba 2023.
Bw Wall alisema kufikia sasa wamefanikiwa kurudisha rotuba kwa zaidi ya hekta 200 za ardhi.