Bayern Munich wajinasia maarifa ya Upamecano baada ya kuwazidi nguvu miamba wa soka ya Uingereza

Bayern Munich wajinasia maarifa ya Upamecano baada ya kuwazidi nguvu miamba wa soka ya Uingereza

Na MASHIRIKA

BAYERN Munich wamewapiku Manchester United, Chelsea, Arsenal na Liverpool kwenye vita vya kumsajili beki mahiri wa RB Leipzig, Dayot Upamecano, 22.

Kwa mujibu wa Hasan Salihamidzic ambaye ni mkurugenzi wa spoti kambini mwa Bayern, beki huyo raia wa Ufaransa atajiunga rasmi na kikosi chake mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa kinara huyo, Bayern wameweka mezani kima cha Sh5.2 bilioni kwa nia ya kumsajili Upamecano kwa mkataba wa miaka mitano.

Taarifa hiyo inatamatisha sasa tetesi nyingi kuhusu mustakabali wa sogora huyo anayechukuliwa kuwa miongoni mwa mabeki bora zaidi kwa sasa katika soka ya bara Ulaya.

Upamecano alifanya maamuzi ya kutua Bayern siku chache baada ya miamba hao wa soka ya Ujerumani na bara Ulaya kutwaa Kombe la Dunia ambalo lilikuwa lao la sita kunyanyua chini ya kipindi cha miezi tisa.

Kutua kwake kambini mwa Bayern kunatarajiwa kumfanya kizibo cha David Alaba anayetarajiwa kuagana rasmi na waajiri wake hao mwishoni mwa msimu huu bila ada yoyote.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

BI TAIFA FEBRUARI 13, 2021

RB Leipzig wamsajili beki Angelino kutoka Manchester City