Bayern Munich wasagasaga Bremer SV kwa mabao 12-0 katika mechi ya German Cup

Bayern Munich wasagasaga Bremer SV kwa mabao 12-0 katika mechi ya German Cup

Na MASHIRIKA

ERIC Maxim Choupo-Moting alifunga mabao manne na kusaidia Bayern Munich kusagasaga Bremer SV inayoshiriki Ligi ya Daraja ya tano nchini Ujerumani kwa mabao 12-0 katika mechi ya raundi ya kwanza ya German Cup mnamo Jumatano usiku.

Ushindi huo ndio mnono zaidi kuwahi kusajiliwa na Bayern chini ya kipindi cha miaka 24 iliyopita.

Choupo-Moting alifungulia Bayern ukurasa wa mabao baada ya dakika nane za kipindi cha kwanza kabla ya Jamal Musiala kufunga goli lake la kwanza kati ya mawili aliyoyapachika wavuni katika mchuano huo.

Jan Warm wa Bremer alijifunga katika 27 kabla ya Bayern walioelekeza makombora 37 langoni, kufungiwa mabao mengine kupitia Malik Tillman, Leroy Sane, Michael Cuisance, Bouna Sarr na Corentin Tolisso. Bayern wanaotiwa makali na kocha Julian Nagelsmann, waliwateremkia wenyeji wao kuanzia dakika ya 76 baada ya mwanasoka Ugo Nobile kuonyeshwa kadi nyekundu.

Ushindi huo ndio mnono zaidi kuwahi kusajiliwa na Bayern tangu 1997 walipowakomoa DJK Waldberg 16-1.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

UhuRuto wazua wasiwasi

Muturi awaambia Wakenya kuwachagua wagombeaji wenye rekodi...