Bayern Munich wasubiri hadi dakika za mwisho kusambaratisha Benfica kwenye gozi la UEFA

Bayern Munich wasubiri hadi dakika za mwisho kusambaratisha Benfica kwenye gozi la UEFA

Na MASHIRIKA

BAYERN Munich walifunga mabao manne katika dakika 20 za mwisho wa kipindi cha pili na kupepeta Benfica 4-0 katika mechi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) iliyowashuhudia wakifungua mwanya wa alama tano kileleni mwa Kundi E.

Leroy Sane aliyepachika wavuni magoli mawili, alifungulia Bayern ukurasa wa mabao katika dakika ya 70 kabla ya kutikisa nyavu za wenyeji wao dakika 14 baadaye. Mabao mengine ya Bayern yalifumwa wavuni kupitia Sousa Soares wa Benfica aliyejifunga katika dakika ya 80 kabla ya Robert Lewandowski kucheka na nyavu dakika mbili baadaye.

Benfica walipoteza nafasi mbili za wazi za kurejea mchezoni mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya Darwin Nunez na Dogo Goncalves kushindwa kumzidi ujanja kipa Manuel Neuer.

Matokeo hayo yanamaanisha kwamba Bayern kwa sasa wanaselelea kileleni mwa Kundi E kwa alama tisa, tano kuliko nambari mbili Benfica. Barcelona wanakamata nafasi ya tatu kwa pointi tatu, mbili zaidi kuliko Dynamo Kyiv.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Ansu Fati sasa kuchezea Barcelona hadi 2027

Afisa aliyetumia cheti feki kupanda cheo atupwa jela

T L