Bayern na Salzburg nguvu sawa katika mkondo wa kwanza wa UEFA

Bayern na Salzburg nguvu sawa katika mkondo wa kwanza wa UEFA

Na MASHIRIKA

MABINGWA mara sita wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) walihitaji bao la dakika za mwisho kutoka kwa fowadi Kingsley Coman ili kuepuka kichapo kutoka RB Salzburg ya Austria katika mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya kipute hicho msimu huu.

Coman alisawazishia Bayern katika dakika ya 90 baada ya kushirikiana vilivyo na Thomas Muller. Awali, Chukwubuike Adamu alikuwa amewaweka Salzburg kifua mbele katika dakika ya 21.

Salzburg wananogesha hatua ya 16-bora ya UEFA kwa mara ya kwanza katika historia. Walijibwaga ugani wakiwa na kiu ya kudhalilisha Bayern waliokuwa wakicheza siku nne baada ya limbukeni VfL Bochuma kuwapokeza kichapo cha 4-2 katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

Iwapo wangechapwa, ingekuwa mara ya kwanza tangu 2019 kwa Bayern kupoteza mechi mbili mfululizo. Chini ya kocha Julian Nagelsmann, Bayern walifuzu kwa hatua ya 16-bora ya UEFA baada ya kushinda mechi zote sita za raundi ya makundi.

Salzburg waliwajibisha kikosi kichanga zaidi katika UEFA kwa mara ya kwanza tangu Ajax ya Uholanzi ifanye hivyo mnamo 2003.

You can share this post!

Levante yaduwaza miamba Atletico Madrid ligini

Liverpool guu moja ndani ya robo-fainali za UEFA baada ya...

T L