Lewandowski aongoza Bayern kuzamisha Benfica na kufuzu kwa 16-bora UEFA

Lewandowski aongoza Bayern kuzamisha Benfica na kufuzu kwa 16-bora UEFA

Na CHRIS ADUNGO

ROBERT Lewandowski alifunga mabao matatu katika mchuano wake wa 100 kwenye soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na kusaidia waajiri wake Bayern Munich kufuzu kwa hatua ya 16-bora baada ya kupepeta Benfica 5-2 mnamo Jumanne usiku uwanjani Allianz Arena.

Lewandowski alifungulia Bayern ukurasa wa mabao katika dakika ya 24 baada ya kukamilisha krosi ya Kingsley Coman. Nyota huyo nahodha wa Poland alichangia goli la pili ambalo Bayern walifungiwa na Serge Gnabry katika dakika ya 32.

Ingawa Rodrigues da Silva Morato alirejesha Benfica mchezoni katika dakika ya 38, Leroy Sane alifungia Bayern bao la tatu mwanzoni mwa kipindi cha pili kabla ya Lewandowski kupachika wavuni magoli mawili zaidi kunako dakika za 61 na 84 mtawalia. Bao la pili la Benfica lilijazwa kimiani na Darwin Nunez katika dakika ya 74.

Kufikia sasa, Lewandowski amefunga mabao 81 kwenye kipute cha UEFA na anajivunia kupachika wavuni mabao matatu katika mechi moja mara nne kutokana na michuano 100 iliyopita.

Amerfungia Bayern magoli 22 kutokana na mechi 18 za hadi kufikia sasa katika mapambano yote ya msimu huu – yakiwemo magoli manane kutokana na michuano minne ya UEFA.

Bayern ambao wameshinda mechi zote nne za Kundi E katika UEFA msimu huu, wanajivunia rekodi ya kufunga mabao 17 kwenye hatua hiyo na wametia kapuni alama 12, sita zaidi kuliko nambari mbili Barcelona. Benfica wanakamata nafasi ya tatu kundini kwa pointi nne, tatu zaidi kuliko Dynamo Kyiv.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Kansa ya matiti: Wanaume msiipuze!

Barcelona wapepeta Dynamo Kyiv na kunusia hatua ya 16-bora...

T L