Lewandowski afunga mabao mawili na kusaidia Bayern kuzamisha Dortmund ligini

Lewandowski afunga mabao mawili na kusaidia Bayern kuzamisha Dortmund ligini

Na MASHIRIKA

FOWADI Robert Lewandowski alipachika wavuni mabao mawili na kusaidia waajiri wake Bayern Munich kusajili ushindi wa 3-2 dhidi ya Borussia Dortmund katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) ugani Westfalenstadion katika gozi la Der Klassiker.

Ushindi huo uliwezesha Bayern kufungua pengo la alama nne kileleni mwa jedwali. Mabingwa hao watetezi wa Bundesliga sasa wanajivunia alama 34 kutokana na mechi 14 zilizopita.

Lewandowski ambaye ni raia wa Poland alifungia Bayern bao la ushindi kupitia penalti iliyosababishwa na Mats Hummels wa Dortmund aliyenawa mpira ndani ya kijisanduku chao.

Awali, Julian Brandt alikuwa amewaweka Dortmund kifua mbele katika dakika ya tano kabla ya Lewandowski kuwarejesha Bayern mchezoni dakika nne baadaye.

Kingsley Coman alipachika wavuni bao la pili la Bayern katika dakika ya 44 kabla ya Erling Braut Haaland kusawazisha mambo mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Goli la Lewandowski lilikuwa lake la 66 kutokana na mechi 55 za mwaka huu wa 2021 na la 118 kutokana na mechi za ugenini kwenye Bundesliga.

Kocha Marco Rose wa Dortmund alionyeshwa kadi nyekundu katika mchuano huo kwa kulalamikia matukio tata ya waamuzi wa mechi hiyo.

Pigo jingine kwa Dortmund waliokuwa wakichezea katika uwanja wao wa nyumbani wa Signal Iduna Park ni jeraha la kichwa alilolipata Brandt baada ya kugongana na beki Dayot Upamecano.

MATOKEO YA BUNDESLIGA (Jumamosi):

Dortmund 2-3 Bayern Munich

Mainz 3-0 Wolfsburg

Leverkusen 7-1 Furth

Arminia 1-1 Cologne

Augsburg 2-3 Bochum

Hoffenheim 3-2 Frankfurt

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

MALEZI KIDIJITALI: Wazazi wawe mfano mzuri wa vifaabebe!

Balozi wa zamani ajiunga na siasa

T L