BB Erzumspor anayochezea Johanna Omolo yaendelea kufufuka Ligi Kuu Uturuki

BB Erzumspor anayochezea Johanna Omolo yaendelea kufufuka Ligi Kuu Uturuki

Na GEOFFREY ANENE

Buyuksehir Belediye Erzumspor anayochezea Mkenya Johanna Omolo inaendelea kujikokota polepole kutoka maeneo hatari ya kutemwa baada ya kukamilisha mechi nne bila kupoteza kwenye Ligi Kuu ya Uturuki, Jumatano.

Erzumspor, ambayo ilichapa Kasimpasa (Januari 18) na Ankaragucu (Januari 31) na kutoka sare dhidi ya Alanyaspor (Januari 21) katika michuano mitatu ya kwanza ya Omolo, ilijiongezea alama moja muhimu katika sare tasa mikononi mwa wenyeji Sivasspor hapo Februari 3.

Hii ilikuwa mechi ya nne ya kiungo huyo wa timu ya taifa ya Harambee Stars tangu agure Cercle Brugge inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Ingawa Sivasspor ilikuwa na umilikaji mkubwa kwa mpira (asilimia 55 dhidi ya 45), timu hizo zilitoshana katika idara nyingi zikiwemo shuti zilizoelekezwa kwa makipa 3-3, uhakika wa pasi zao asilimia 75 kila mmoja, ikabu 19-19, kadi za njano 1-1 na kuotea langoni 2-2.

Erzumspor ilipata shuti moja zaidi ya Sivasspor 9-8. Fenerbahce inaongoza jedwali kwa alama 48. Sivasspor ni ya 14 kwa alama 25 nayo Erzumspor inakamata nafasi ya 18 alama nne nyuma kwenye ligi hiyo ya timu 21.

You can share this post!

Broadways yazindua mkate usio na sukari

Wanaojiita ‘mahasla’ kusukumwa jela