Habari Mseto

Bei ya gesi yazidi kupaa

November 22nd, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Bei ya gesi ya kupika inaendelea kupanda licha ya serikali kuondoa ushuru kwa bidhaa hiyo.

Kwa miezi 27 mfululizo, bei ya gesi imekuwa ikipanda. Kulingana na takwimu, kununua gesi ya mtungi wa kilo 13 iliongezeka hadi Sh2,187 Septemba kutoka Sh2,170 Juni na Sh2,073 Julai mwaka jana.

Tangu 2016 wakati serikali iliondoa ushuru kwa gesi, bei ya Septemba ndio ya juu zaidi. Serikali iliondoa ushuru huo kwa lengo la kuvutia wananchi wa mapato ya chini kumudu gesi ili kudhibiti matumizi ya mafuta ya taa na makaa kupika.

Kwa muda, bei ilikuwa ni Sh2, 231 Juni 2016 ambapo ilianguka hadi Sh2, 000 Oktoba 2016.

Lakini bei hiyo imekuwa ikipanda tangu Agosti 2017 kulingana na shirika la takwimu nchini (KNBS).