Beki Raphael Varane wa Man-United astaafu soka ya kimataifa

Beki Raphael Varane wa Man-United astaafu soka ya kimataifa

Na MASHIRIKA

BEKI matata wa Manchester United, Rapahel Varane, amestaafu soka ya kimataifa akiwa na umri wa miaka 29.

Varane aliyesaidia timu ya taifa ya Ufaransa kunyanyua ubingwa wa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, alifungia miamba hao mabao matano kutokana na mechi 93 tangu aanze kuwajibishwa mwaka wa 2013.

Mechi yake ya mwisho kambini mwa Ufaransa ilikuwa dhidi ya Argentina kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2022 iliyoshuhudia Argentina ikifunga penalti 4-2 baada ya sare ya 3-3.

Varane aliyesajiliwa na Man-United kutoka Real Madrid mnamo Agosti 2021 anaangika daluga zake kimataifa mwezi mmoja baada ya kipa na nahodha wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris, kustaafu soka ya kimataifa wiki tatu tangu Ufaransa izamishwe katika Kombe la Dunia.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Leliman ahukumiwa kunyongwa kwa mauaji ya wakili Willie...

Dereva Karan kuanza kutetea taji la mbio za magari kitaifa...

T L