Beki wa timu ya taifa ya Uturuki afariki dunia akiwa na umri wa miaka 27

Beki wa timu ya taifa ya Uturuki afariki dunia akiwa na umri wa miaka 27

Na MASHIRIKA

DIFENDA wa timu ya taifa ya Uturuki, Ahmet Calik, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 27.

Hadi kufa kwake, Calik aliyehusika katika ajali ya barabarani mnamo Jumanne, alikuwa akichezea klabu ya Konyaspor katika Ligi Kuu ya Uturuki (Turkish Lig). Aliwahi pia kuvalia jezi za Galatasaray nchini Uturuki kwa miaka mitatu.

“Tunasikitishwa na kifo cha Calik ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wetu tangu siku ya kwanza alipojiunga na Konyaspor,” ikasema sehemu ya taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.

Uchunguzi kuhusu kiini cha ajali hiyo tayari umeanzishwa na mamlaka husika nchini Uturuki.

Calik alianza kupiga soka ya kulipwa kambini mwa Genclerbirligi. Alichezea Galatasaray zaidi ya mechi 50 katika kipindi cha misimu mitatu kabla ya kujiunga na Konyaspor mnamo 2020 ambapo aliwajibishwa mara 51.

Beki huyo alichezea timu ya taifa mara nane kati ya 2015 na 2017 baada ya kuchezeshwa mara kadhaa katika timu za chipukizi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Chelsea warefusha mkataba wa beki Thiago Silva kwa mwaka...

AFCON: Limbukeni Sierra Leone waridhika kutoka sare na...

T L