Beki wa zamani wa Liverpool, Maxi Rodriguez, astaafu soka

Beki wa zamani wa Liverpool, Maxi Rodriguez, astaafu soka

Na MASHIRIKA

FOWADI wa zamani wa Liverpool, Maxi Rodriguez, ameangika rasmi daluga zake za usogora akiwa na umri wa miaka 40.

Nyota huyo aliyewahi kuchezea Liverpool kati ya 2010 na 2012, alistahiwa kwa heshima kubwa baada ya mashabiki wote uwanjani kumsimamia wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Argentina iliyowashuhudia wakiambulia sare dhidi ya Banfield.

Fataki zililipuliwa uwanjani Rodriguez alipokuwa akishangiliwa na wanasoka wa pande zote mbili. Supastaa wa Argentina Lionel Messi, nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson na Luis Suarez wa Atletico Madrid, ni miongoni mwa wachezaji waliotumia mitandao yao ya kijamii kumpongeza Rodriguez.

Sawa na Rodriguez, Messi pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichowakilisha Argentina kwenye fainali za Kombe la Dunia za 2014 nchini Brazil.

You can share this post!

Kesi ya ufisadi ya Sh7.4Bn dhidi ya Mbunge Rigathi Gachagua...

Bellingham apigwa faini ya Sh5.3 milioni kwa kukosa maamuzi...

T L