Michezo

Bellerin tabasamu kokote aendako baada ya kujinasia mrembo Mhindi

February 12th, 2018 2 min read

BEKI matata wa Arsenal, Hector Bellerin akiwa na mwanamitindo maarufu mzawa wa India, Shree Patel, 31. Picha/ Hisani

Na MASHIRIKA

Kwa Muhtasari:

  • Bellerin alionekana akiponda raha na kichuna Shree ambaye anafahamika kwa wepesi wake wa kujilegeza kimapenzi kwa wanasoka
  • Beki huyo alikiri kupagawishwa na urembo wa king’asti huyo
  • Esha alijitokeza peupe kuusifia utendakazi wa Bellerin kitandani na kumbeza Sanchez wa Man United

BEKI matata wa Arsenal, Hector Bellerin sasa kajinasia penzi la msomi na mwanamitindo maarufu mzawa wa India, Shree Patel, 31.

Nyota huyo alionekana wiki iliyopita akiponda raha na kichuna huyo ambaye anafahamika sana kutokana na wepesi wake wa kujilegeza kimapenzi kwa wanasoka chipukizi wenye pumzi zisizokwisha haraka uwanjani na chumbani.

Pindi baada ya kukatiza uhusiano wake na mwigizaji shupavu wa Bollywood, Esha Gupta yapata miezi 10 iliyopita, Bellerin, 22 alitumia mtandao wake wa Instagram kuanzisha mawasiliano na Shree, kichuna anayeaminika kuwa chanzo cha kusambaratika kwa penzi lililompa difenda huyo wa Uhispania hifadhi moyoni mwa Esha aliyekuwa akimfungulia Alexis Sanchez mzinga wake wa asali kabla ya kuvutiwa na umachachari wa Bellerin.

 

Doa

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, uhusiano wa Bellerin na Esha ambaye ni malkia wa zamani wa taji la Miss India ulianza kuingia baridi mnamo Aprili 2017 baada ya beki huyo kukiri kuteswa na penzi la Shree ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ukachero.

Mbali na kufichua kwamba humlazimu mara kwa mara kumpangia Shree safari za siri kwa lengo la kumpiga moyo pasi, Bellerin pia alikiri kupagawishwa na urembo wa kichuna huyo.

Japo Bellerin amekiri kuwa yake na Esha mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa ni ya kuzikika katika kaburi la sahau, mwanasoka huyo amesisitiza kuwa watasalia kuwa marafiki tu wa kawaida huku “kila mmoja akijiendeshea maisha yake apendavyo.”

 

Usogora wa Bellerin kitandani

Ikumbukwe kwamba uhusiano bora uliotawala urafiki wa Bellerin na Sanchez aliyehamia majuzi Manchester United nusura usambaratishwe baada ya kutiwa doa na Esha aliyejitokeza peupe kuusifia utendakazi wa Bellerin kitandani na kumbeza Sanchez aliyedokoa tunda lake kwa zaidi ya miaka miwili kwa kumlinganisha na gumegume lisiloelewa maana ya kumridhisha kidosho chumbani”.

Kukomaa kwa penzi kati ya Shree na Bellerin kunajiri miezi michache tu baada ya sogora huyo kutemana na mwigizaji na mwanamitindo maarufu waLondon, Isabelle Johnson-Ewers na uhusiano wake na kipusa Berta Requeno kusambaratika ulipingiliwa na mdudu.