Bellingham apigwa faini ya Sh5.3 milioni kwa kukosa maamuzi ya refa uwanjani

Bellingham apigwa faini ya Sh5.3 milioni kwa kukosa maamuzi ya refa uwanjani

Na MASHIRIKA

KIUNGO raia wa Uingereza na klabu ya Borussia Dortmund, Jude Bellingham, amepigwa faini ya Sh5.3 milioni na Shirikisho la Soka la Ujerumani kwa hatia ya kukosoa uteuzi wa refa Felix Zwayer kusimamia mechi iliyowakutanisha na Bayern Munich katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

Bellingham alimchemkia Zwayer na kukosoa baadhi ya maamuzi yake kwenye mchuano huo uliokamilika kwa Bayern kushinda 3-2. Kiungo huyo pia alirejelea kisa kilichowahi kumshuhudia Zwayer akipigwa marufuku ya miezi sita kwa hatia ya kupanga matokeo ya mechi mnamo 2005.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Ujerumani, Bellingham amepigwa faini kwa kosa la kudhihirisha mienendo isiyokuwa ya uanaspoti mwema. Dortmund wameshikilia kwama hawatakata rufaa kulalamikia ukubwa wa kiasi cha adhabu ambayo Bellingham amepokezwa.

Wakati wa mechi, Zwayer alipuuza kilio cha Dortmund waliodai penalti kabla ya wageni wao kupewa baada ya Mats Hummels kunawa mpira ndani ya kijisanduku. Robert Lewandowski alipachika wavuni penalti hiyo na kuvunia Bayern ushindi.

Bellingham aliingia katika sajili rasmi ya Dortmund mnamo Julai 2020 baada ya kubanduka kambini mwa Birmingham City kwa kima cha Sh4.6 bilioni.

You can share this post!

Beki wa zamani wa Liverpool, Maxi Rodriguez, astaafu soka

Sharks, Homeboyz zalenga kupanua uongozi ligini leo

T L