Habari Mseto

Benki ya Co-op inavyounda mabilioni kutokana na mikopo

May 26th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Benki ya Cooperative imepata ongezeko la faida kwa asilimia 6.25 kwa miezi mitatu hadi Machi 2018.

Ongezeko hilo lilitokana na ongezeko la mikopo iliyochukuliwa na wateja. Faida baada ya ushuru ilikuwa ni Sh3.4 bilioni ikilinganishwa na Sh3.2 bilioni katika robo ya mwanzo ya mwaka jana.

Mapato kutokana na riba yaliongezeko la asilimia 9 hadi Sh7.4 bilioni, ilhali mapato kutokana na riba ya dhamana ya serikali iliongezeka kwa asilimia 13.4 hadi Sh2 bilioni.

Kulingana na benki hiyo, faida hiyo imetokana na hali inayoendelea kuimarika kutokana na hali mbaya kibiashara iliyoshuhudiwa mwaka jana kwa sababu ya uchaguzi.

Mapato yasiyo ya faida yaliongezeka hadi Sh3.52 bilioni ikilinganishwa na Sh3.39 bilioni katika kipindi hicho 2017.