Habari Mseto

Benki zakaidi kupunguzia wateja riba ya mikopo

August 21st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

LICHA ya Benki Kuu ya Kenya kushusha kiwango cha riba, benki za humu nchini zimekataa kupunguza riba kwa wateja wake.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa CBK, ambayo ilisema wateja wengi, katika uchunguzi uliofanywa Julai, walisema kuwa benki zilifanyia mikataba ya mikopo marekebisho ili wateje wake waendelee kulipa viwango vya zamani.

“Waliohojiwa walisema kulikuwa na changamoto kuhusiana na usimamizi wa mikopo baada ya kiwango cha riba kushukis hwa,” CBK ilisema katika ripoti ya uchunguzi huo.

“Baadhi ya benki zilifupisha kipindi cha kulipa na kuacha kiwango cha malipo ilivyokuwa awali, hivyo kutowasaidia wateja wake,” iliongeza CBK katika ripoti hiyo.

Mwezi Julai, CBK ilishusha kiwango cha riba kwa asilimia 0.5 kutoka asilimia 10 hadi asilimia 9.5.

Ilitarajiwa kuwa hatua hiyo ingezifanya benki kupunguza kiwango cha riba kwa asilimia kama hiyo kwa wateja wake.

Kwa sasa, benki zinatoza mikopo kwa wateja wake riba ya asilimia 14, hivyo kufuatia mabadiliko hayo, benki zinafaa kutoza sio zaidi ya asilimia 13.5.