Habari Mseto

Benson Mutura atajwa Spika wa Nairobi

August 16th, 2020 1 min read

 COLLINS OMULO na FAUSTINE NGILA

Mbunge wa zamani wa Makadara Benson Mutura ameteuliwa kuwa spika wa bunge la Nairobi baada ya kupata kura 99 kati ya 122 kwenye raundi ya kwanza.

Kura hizo zilifanywa kupitia mtandao wa Zoom ksababu ya njia zilizowekwa ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona .

Bw Mutura aliwashinda watu wengine watano kumrithi Bi Beatrice Elachi aliyejiuzulu Jumatano..

Akitangaza matokeo ya kura hizo spika aliyeshikilia John Kamangu alisema,Natangaza ushindi wa Benson Mutura kuwa spika mpya ka bunge ya kati ya Nairobi ambaye amepata kura Zaidi ya thuluthi mbili ya kura zilizopingwa.

Spika huyo aliwashukuru Rais Uhuru Kenyatta ,chama cha Jubilee na wapinzabi kwa kuwa na Imani naye na kuhaidi kufanya kuwafanyia kazi wote na kuwasikiza bila ubaguzi

Bw Mutura alihahirisha vikao vya bunge hio hadi Septemba 8 bada ya kuchukua usukani kutoka kwa spika aliyeshikilia ambaye ni naibu Spiuka John Kamangu.