Michezo

Benzema afunga mawili na kusaidia Real Madrid kupepeta Bilbao katika La Liga

December 16th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

KARIM Benzema alifunga mabao mawili na kusaidia Real Madrid kuwapokeza Athletic Bilbao kichapo cha 3-1 mnamo Disemba 15, 2020.

Ni ushindi ambao ulishuhudia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) wakipaa hadi kileleni mwa jedwali kwa alama 26 sawa na Atletico Madrid na Real Sociedad.

Nyota Raul Garcia wa Bilbao alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 13 baada ya kumchezea visivyo kiungo Toni Kroos visivyo.

Kroos ndiye aliyewafungulia Real ukurasa wa mabao katika dakika ya 45 kabla ya Benzema kuongeza mawili katika dakika za 74 na 92 mtawalia.

Bao la pekee kwa upande wa Bilbao lilipachikwa wavuni na Ander Capa aliyeshirikiana vilivyo na Mikel Vesga kumtatiza kipa Thibaut Courtois mara kadhaa katika kipindi cha pili.

Real kwa sasa wamesajili ushindi kutokana na mechi nne zilizopita mfululizo katika mashindano yote.