Bertrand ajiunga na Leicester baada ya kandarasi yake na Southampton kuisha

Bertrand ajiunga na Leicester baada ya kandarasi yake na Southampton kuisha

Na MASHIRIKA

BEKI wa pembezoni kushoto, Ryan Bertrand amejiunga na Leicester City kwa mkataba wa miaka miwili bila malipo, baada ya kuondoka Southampton mkataba wake ulipotamatika.

Bertrand, 31, aliyeyoyomea Leicester Alhamisi 15 Julai, amehudumia Southampton kwa misimu saba na kusakatia timu hiyo jumla ya mechi 240.

Bertrand pia aliwahi kushinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya(Uefa Champions League) akichezea Chelsea. Aliwahi kujumuishwa kwenye kikosi cha Three Lions cha Uingereza, lakini hajahusishwa tangu mwaka 2017.

Bertrand alieleza furaha yake kujiunga na Leicester, akiwasifia kuwa timu iliyopiga hatua mbele, hasa tangu Brendan Rodgers alipotwaa mikoba ya timu hiyo.

“Nina furaha kujiunga na timu hii ya kifahari na nitajitolea kwa kila hali kuhakikisha nimechangia katika kuimarika kwake,” alisema kupitia kwa taarifa.

Leicester, washindi wa kombe la F.A msimu jana watagaragazana na Manchester City, mshindi wa ligi katika kipute cha Community Shield.

Wataanza kampeni za ligi kuu Agosti 14, ambapo watavaana na Wolverhampton Wanderers nyumbani King Power Stadium.

TAFSIRI NA: NDUNGI MAINGI

You can share this post!

UMBEA: Si kila wivu ni mbaya, wakati mwingine hujenga...

Karo: Magoha aonya walimu akiwataka kutofukuza wanafunzi