Betis wadidimiza matumaini ya Real Madrid kuhifadhi ufalme wa La Liga msimu huu

Betis wadidimiza matumaini ya Real Madrid kuhifadhi ufalme wa La Liga msimu huu

Na MASHIRIKA

MATUMAINI ya Real Madrid kuhifadhi ubingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) msimu huu yalididimizwa na Real Betis mnamo Jumamosi baada ya kulazimishiwa sare tasa uwanjani Alfredo Di Stefano.

Chini ya kocha Zinedine Zidane, Real kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili kwa alama 71, mbili nyuma ya viongozi Atletico Madrid.

Barcelona ambao wana mechi mbili zaidi za kusakata, wanashikilia nafasi ya tatu kwa pointi 68, moja pekee mbele ya Sevilla wanaofunga orodha ya nne-bora.

Vinicius Rodrygo nusura afungie Real bao la ushindi mwishoni mwa kipindi cha pili ila juhudi zake zikaambulia pakavu baada ya kombora alilomwelekezea kipa wa Betis kugonga mwamba wa goli.

Chini ya kocha Manuel Pellegrini ambaye ni raia wa Chile, Betis kwa sasa wanashikilia nafasi ya sita kwa alama 50 sawa na Real Sociedad ambao pia wanafukuzia fursa ya kufuzu kwa soka ya Europa League msimu ujao.

Guido Rodriguez wa Betis naye alimshughulisha vilivyo kipa Thibaut Courtois katika sehemu kubwa ya kipindi cha pili.

Nafuu zaidi kwa Real waliowapiga Cadiz mnamo Aprili 21 katika mechi nyingine ya La Liga na kutua kileleni mwa jedwali ni marejeo ya kiungo mvamizi Eden Hazard ambaye amepona jeraha.

Nyota huyo raia wa Ubelgiji aliletwa uwanjani katika dakika ya 77 katika mchuano wake wa kwanza ligini akivalia jezi za Real tangu Machi 13, 2021.

Real kwa sasa wanajiandaa kupepetana na Chelsea katika mchuano wa mkondo wa kwanza nusu-fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Aprili 27, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

JAMVI: Katika hizi ziara zake Oparanya ni ‘fuko’ au ni...

JAMVI: Kibarua kwa Ruto Mlimani Tangatanga wakitunga...