Habari Mseto

'Biashara ndogo, watu binafsi wamelemewa kulipa madeni ya benki'

August 25th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

DENI kubwa katika benki za humu nchini lilitokana na mikopo kwa watu binafsi na biashara ndogo.

Deni hilo la Sh264.6 bilioni lilikadiriwa 2017, kuonyesha jinsi uchumi ulivyoathiriwa.

Ripoti hiyo ni kwa mujibu wa Benki Kuu nchini (CBK), iliyoonyesha kuwa watu binafsi walishindwa kulipa deni la Sh121.4 bilioni 2017, ambalo lilikuwa asilimia 45.89 ya deni lote katika sekat hiyo.

Ripoti hiyo ilibaini kuwa watu wengi wanachukua mikopo wasio na uwezo wa kuilipa, zaidi ya kuonyesha jinsi biashara zinafanya vibaya.

Moja ya sababu ya biashara kufanya vibaya inatokana na kucheleweshwa kwa malipo na serikali za kaunti na ile kitaifa baada ya kupewa huduma au bidhaa.