Biashara ya mkojo wa wajawazito yanoga TZ

Biashara ya mkojo wa wajawazito yanoga TZ

Na MWANDISHI WETU

MKOJO wa wajawazito umegeuka biashara kubwa Tanzania baada ya kusemekana kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa ya binadamu.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi nchini humo kwa siku 14, umebainisha kuwa ukusanyaji wa mikojo hiyo huwa unafanyika kwa usiri mkubwa jijini Dar es Salaam.

Wajawazito hufuatwa majumbani na kushawishiwa kukubali kuuza mikojo yao ambayo hutumiwa kwa utengenezaji wa dawa.

Imebainika kuwa kampuni ya Polai (TZ) huinunua mikojo ya wajawazito kwa maelezo kuwa ni tiba ya magonjwa mbalimbali ya binadamu.

Mikojo hiyo hukusanywa na huwekwa kwenye vikopo kisha kupelekwa katika nyumba iliyopo Mtaa wa Mferejini Kata ya Manzese, kabla ya kupelekwa kwa raia wa kigeni anayetajwa kuwa mmiliki wa kampuni hiyo.

Kulingana na tovuti ya Polai, kampuni hiyo imehudumu China na Taiwan kwa zaidi ya miaka 40, na hujihusisha katika utafiti na utengenezaji wa mali asili zinazotumiwa kutengeneza dawa za kutibu mgando wa damu ubongoni, shinikizo la damu na utasa.

You can share this post!

Thirdway lawamani kuhusu kesi inayopinga BBI

Wakazi sasa kusafisha jiji kila mwezi