Habari Mseto

Biashara yanoga Nakuru wafuasi wa Owuor wakijiandaa kwa krusedi

December 22nd, 2018 1 min read

Na MAGDALENE WANJA

Shughuli zilisimama kwa muda mrefu katika mji wa Nakuru baada ya wafuasi wa nabii Dkt David Owuor kumiminika kutangaza mkutano unaotarajiwa kufanyika.

Walioathirika zaidi ni wenye magari, bodaboda, texi na pia wapiti njia kwani umati huo wa wafuasi ulitapakaa kila pahali.

Ata hivyo wachuuzi walipata nafuu kwani walichukua nafasi hiyo kuwauzia waumini hao vitambaa vya kufuta jasho.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika eneo la Menengai grounds.

Walibeba mabango yenye jumbe mbalimbali huku wakiimba nyimbo na matangazo, wafuasi wa nabii huyo walipita katikati ya mji wakiwaalika wakazi kuhudhuria mkutano

Kulingana na wafuasi hao, mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 29 hadi 31 Desemba 2018 huku wakiongeza kuwa nabii huyo atafanya miujiza.

Hii ni mara ya pili ambapo nabii huyo anafanya mkutano katika mji wa Nakuru mwaka huu.