Biden akemea Otrega kuwafunga wapinzani wake

Biden akemea Otrega kuwafunga wapinzani wake

WASHINGTON, Amerika

Na AFP

Rais Joe Biden wa marekani ameushutumu uchaguzi wa urais Nicaragua akisema ulikuwa “mzaha”, huku rais wa sasa Daniel Ortega akitarajiwa kushinda kwa kishindo baada ya kuwazuia wapinzani kushindana naye.

Kwenye taarifa, Ikulu ya White House iliutaja uchaguzi huo kuwa dhihaka.“Utawala wa Ortega umeiba uchaguzi huu hata kabla ya siku ya kura kwa kuwafunga wapinzani 39. Wapinzani hao ni pamoja na saba ambao wangeshiriki kuwania urais,” akasema Bw Biden.

Alimkashifu rais huyo wa Nicaragua kwa kuzima vyombo huru vya habari, wadau wa sekta ya kibinafsi na mashirika ya kijamii.“Kwa kukwamilia mamlakani kwa miaka mingi, familia ya Ortega na Murillo sasa wanatawala Nicaragua kama mamluki.

”Raia wa Nicaragua walienda uchaguzini Jumapili chini ya kile ambacho mashirika ya kutetea haki za binadamu yametaja kuwa hali ya taharuki na hofu.Vituo vya kura vilifungwa saa kumi na mbili jioni, baada ya shughuli ya mchana kutwa chini ya ulinzi wa maafisa 30,000 wa polisi na jeshi.

Ortega, 75, anatarajiwa kuchukua mamlaka kwa kipindi cha nne mfululizo pamoja na mkewe Murillo, 70.

You can share this post!

Kuna hatari ya Raila ‘kujikwaa’ kisiasa kwa kumtetea...

Wazee wakemea viongozi kunyamazia mzozo wa bahari

T L