Biden hajapona corona, daktari wake asema

Biden hajapona corona, daktari wake asema

NA MASHIRIKA

WASHINGTON, Amerika

RAIS wa Amerika Joe Biden hajapona Covid-19 lakini anahisi vizuri bila joto jingi mwilini, asema daktari wake Dkt Kevin O’Connor.

O’Connor alisema Jumatano kwenye taarifa kwamba alifanya mazoezi mepesi kabla ya kupimwa siku hiyo jioni.

Hata hivyo, daktari alisema Rais Biden anakumbwa na kikohozi, lakini sio kila wakati.

“Kiwango chake cha joto, presha ya damu, kupiga kwa moyo, kupumua na kiwango cha oksijeni kwenye damu ni sawa. Aidha, hali ya mapafu yake ni sawa,” amesema.

Rais huyu wa Amerika ataendelea kutengwa huku akiendelea kupata afueni. Alipatikana na Covid-19 mnamo Julai 30.

Ikulu ya White House ilisema kuwa licha ya kuugua corona, Biden angali anaendelea kufanya kazi kutoka katika makazi yake rasmi.

Aidha, Biden anajihadhari asije akawaambukiza wafanyakazi katika makazi yake, maafisa wa shirika la ujasusi (CIA) au wafanyakazi wa Ikulu ambao kazi yao inawahitaji kuwa karibu na rais huyo.

Rais Biden alipatikana na Covid-19 kwa mara ya kwanza mwishoni mwa Juni. Alirejelea shughuli za kawaida mnamo Julai 27.

Tangu alipopatikana na corona tena, Biden amelazimika kufutilia mbali mipango yake ya kuzuru Michigan na jimbo la Dalaware anakotoka.

Mnamo Agosti 1, 2022 aliwahutubia wanahabari wachache kutoka umbali, kuhusiana na mauaji wa aliyekuwa kiongozi wa Al Qaeda Ayman al-Zawahiri.

TAFSIRI: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa Everton fowadi tegemeo Dominic Calvert-Lewin...

Wawira ashindia Kenya medali ya shaba Birmingham unyanyuaji...

T L