Biden, Putin kujadiliana taharuki ya Marekani, urusi kuhusu Ukraine

Biden, Putin kujadiliana taharuki ya Marekani, urusi kuhusu Ukraine

RAIS Joe Biden wa Amerika na mwenzake Vladimir Putin wa Urusi, kesho watazungumza kwa njia ya simu, kujadili taharuki iliyopo kati ya nchi hizo mbili kuhusu Ukraine.

Mazungumzo hayo yanajiri siku kadhaa baada ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Amerika, Antony Blinken, kudai kwamba Amerika ina ushahidi wa kutosha kuonyesha Urusi inapanga kuishambulia Ukraine.

Hata hivyo, aliongeza kuwa si wazi ikiwa Rais Putin amefanya uamuzi kulivamia taifa hilo.Amerika imekuwa ikiilaumu Urusi kwa “kuivamia” Ukraine, huku ikidai itafanya kila iwezalo kuitetea dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Ukraine inasema Urusi imetuma majeshi 94,000 mpakani mwake.

You can share this post!

OKA, Raila wataungana kukabili Ruto 2022 – Lenku

Arati akana dai la kuzua fujo kanisani

T L