Binti adai kupigwa sababu hajakeketwa

Binti adai kupigwa sababu hajakeketwa

Na Oscar Kakai

MWANAMKE wa miaka 22 kutoka kata ya Murpus, Pokot Magharibi anatafuta haki kwa madai ya kupigwa na kuumizwa na wanawake wenzake sababu hajakeketwa.

Msichana huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Upili ya Werpo Ortum, alisema kuwa amekuwa akipitia unyanyapaa mara nyingi na kutusiwa kuwa hastahili kuongea mbele ya wanawake wengine sababu hajakeketwa.

Kwenye kikao cha wiki cha chama siku ya Jumapili katika boma la jirani wake mambo yalienda segemnege baada ya wanawake wanzake walipomvamia na kumtandika na hata kumuuma kidole gumba na kumshutumu kwa kuwakilisha maoni yao ili hali hajakeketwa.

Akiongea na Taifa Leo kwa njia ya simu, mwanamke huyo Bi Sylvia Chepting alisema kuwa mnamo Jumapili kwenye mkutano huo wa chama alipendekeza kuwa wanawake wenzake wawe wakija mapema sababu yeye ni mwanafunzi na na kazi ya shule na suala hilo halikumfurahisha mmjoa wa majirani zake.

“Jirani alikuja kama amechelewa na nikamuuliza sababu lakini alinigeuka na kuninyamazisha akiasema kuwa ninafaa kukeketwa kabla ya kuongea mbele yao. Alinivamia na mangumi na mateke,” alisema.

Bi Chepting aliongeza kusema kuwa mwanamke huyo alimuuma kidole gumba na kumwambia kuwa atampeleka kwa mkeketaji ili apashwe tohara.

“Majirani wengine waliokoa maisha yangu sababu nilikuwa napiga nduru nikiomba msaada na nikamwambia nitamripoti kwa chifu. Majirani waliniokoa na hata Jumatatu sikuenda shuleni sababu nilikuwa nikiumia kutokana na majeruhi,” alisema.

You can share this post!

Wauguzi wagomea chanjo ya corona licha ya amri kali

Onyo kwa wanahabari kuhusu ripoti za kisiasa