BKPL: Mathare United kuwinda alama tatu

BKPL: Mathare United kuwinda alama tatu

Na JOHN KIMWERE
HUKU zikiwa zimesalia mechi sita kukamilisha ratiba yake katika kipute cha Ligi Kuu ya Betking Kenya Premier League (BKPL), Mathare United leo itaingia mzigoni kukabili Sofapaka FC kusaka alama tatu muhimu.
Mathare United inayotiwa makali na kocha, Frank Ouna imepania kujituma kiume kusaka alama za kuisaidia kukwepa shoka la kushushwa ngazi. Kocha huyo aliyetwaa mikoba ya kocha, Salim Ali bado ana imani kuwa wanaweza kufanya kweli licha ya kupoteza jumla ya mechi 17, kutoka nguvu sawa mara sita na kushinda michuano mitatu.
”Nina imani wachezaji wangu watajituma bila kulegeza kamba kupigana na wapinzani wetu lengo letu likiwa kuzoa ushindi wa alama tatu ili kujiongezea matumaini ya kufanya vizuri,” kocha wa Mathare alisema na kuongeza kuwa bado haamini kuwa wanaweza kuteremshwa ngazi.
Kwenye mechi ya wikendi Mathare ilinyukwa mabao 2-1 na Wazito. Mathare inaburura mkia kwa kuzoa alama 16 baada ya kushiriki mechi 26 inakofuata Vihiga United ambayo imecheza mechi 27 na kubeba alama 20.
Kwenye ratiba ya leo nayo Kariobangi Sharks ya kocha, William Muluya imepangwa kucheza na Kakamega Homeboyz katika Uwanja wa kilimo mjini Nakuru. Bila shaka mchezo huo unatazamiwa kushuhudia ushindani mkali hasa Sharks itakapokuwa mbioni kuliza kisasi baada ya kilimwa mabao 3-0 na KCB.
  • Tags

You can share this post!

UIGIZAJI: Lynn aamini hatua moja baada ya nyingine...

Diva: Bado nahitaji sapoti kufikia lengo