Black Stars kukosa mazishi ya Christian Atsu

Black Stars kukosa mazishi ya Christian Atsu

JOHN ASHIHUNDU na MASHIRIKA

KIKOSI kizima cha timu ya taifa ya Ghana kitakosa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Christian Atsu aliyekuwa akisakatia klabu ya Hatayspor nchini Uturuki.

Mshambuliaji huyo aliaga dunia nchini Uturuki mwezi uliopita kutokana na tetemeko la ardhi nchini humo pamoja na taifa la Syria atazikwa nyumbani kwao Dogobome, siku ambayo wachezaji wa Black Stars watakuwa wakicheza na Angola katika mechi ya mchujo kuwania ubingwa wa AFCON.

Black Stars itarejea nchini baada ya mazishi hayo, ambapo mastaa Andrew Ayew, Thomas Partey, Jordan Ayew na Daniel Amartey ni miongoni mwa wachezaji kikosi hicho watakaokosa kutoa heshima zao za mwisho siku hiyo.

Alipoulizwa iwapo wachezaji wa Black Stars watahitajika wakati wa mazishi hayo, mmiliki wa klabu ya Cheeter FC iliyogundua kipaji cha Atsu, Abdul Haye Yartey alisema kamwe hawajajumuishwa kwenye ratiba ya siku hiyo.

Yarter aliyegundua kipawa cha Atsu akiwa mdogo na kumpeleka Ureno kujiunga na FC Porto alisema hayo leo akiwa katika afisi ya Wazira ya Vijana na Michezo baada ya kukutana na familia ya marehemu.

“Mipango ya mazishi inakaribia kukamilika na serikali inatarajiwa kuhusika kikamilifu. Tunashirikiana vyema na jamii ya Atsu na kila kitu kinaendelea sawa sawa, kuhakikisha amepewa maziko ya heshima,” Henry Asante Twum aliye kwenye kamati ya mipango ya matanga hayo aliambia waandishi wa habari.

Mshambuliaji huyowa klabu ya Taner Savut mwenye umri wa miaka 31 alikuwa miongoni mwa watu 46,000 waliopoteza maisha yao baada ya poromoka kubwa lilioangusha majengo kadhaa likiwemo alilolkuwa akiishi kusini kwa Uturuki

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea na Newcastle United ambaye mwili wake ulipatikana kwenye vifusi siku 12 baadaye alifahamika zaidi baada ya kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wakati wa fainali za AFCON za 2015 nchini Equatorial Guinea.

Alikuwa katika kikosi cha Black Stars kilichoshiriki katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mnamo 2014.

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo alisema Ghana imepoteza balozi mkubwa wa taifa hilo ambayo itakuwa vigumu kujaza pengo alilowacha.

  • Tags

You can share this post!

Mwenye China Square asema nia yake ni kupunguzia Wakenya...

Wabunge wataja ruzuku ya bei ya unga wakati wa Uhuru kuwa...

T L