Michezo

Black Stars waahidiwa donge nono wakilima Harambee Stars

August 27th, 2018 2 min read

Na Geoffrey Anene

WACHEZAJI wa Black Stars ya Ghana watapokea Sh504,300 kila mmoja timu hiyo ikilemea Harambee Stars katika mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AFCON) mwaka 2019 itakayosakatwa Septemba 8, 2019 katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Tovuti ya GhanaWeb imenukuu msemaji wa kamati ya muda ya pamoja ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Dan Kwaku Yeboah akisema bonasi ya Black Stars kushinda muhimu za kimataifa haitabadilishwa.

Kulikuwa na wasiwasi kwamba kitita hicho kitapunguzwa na kamati ya Yeboah, ambayo imetwikwa majukumu ya kuendesha soka nchini humo baada ya sakata ya ufisadi kugunduliwa katika Shirikisho la Soka la Ghana (GFA) mwezi Juni mwaka 2018. Chama tawala cha New Patriotic Party (NPP) kilipunguza bonasi hii kutoka Sh1,008,500 hadi Sh 504,300 kilipoingia mamlakani mwaka 2016. Black Stars inatarajiwa kupiga kambi ya mazoezi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia siku kadhaa kuanzia Septemba 2 kabla ya kuelekea Kenya.

Tiketi za mchuano kati ya Kenya na Ghana zinauzwa Sh1,000 (VIP) na zile za kawaida Sh200.

Kikosi cha Kenya kinatarajiwa kuingia kambini Septemba 2.

Ghana inaongoza kundi hili kwa alama tatu kutokana na ushindi wake wa mabao 5-0 dhidi ya Ethiopia. Sierra Leone ni ya pili kwa alama tatu baada ya kulima Kenya 2-1. Kenya ya kocha Sebastien Migne na Ethiopia zinashikilia nafasi mbili za mwisho bila pointi. Mshindi wa kundi hili ataingia AFCON mwaka 2019.

Vikosi:

Kenya

Makipa – Ian Otieno (Red Arrows, Zambia), Patrick Matasi (Tusker), Boniface Oluoch (Gor Mahia), Brian Bwire (Kariobangi Sharks), Farouk Shikalo (Bandari);

Mabeki – Brian Mandela (Maritzburg, Afrika Kusini), David Owino (Zesco, Zambia), Joseph Okumu (AFC Ann Arbor, Marekani), Musa Mohammed (Nkana FC, Zambia), Erick Ouma (Vasalund, Uswidi), David Ochieng (IF Brommapojkarna, Uswidi), Abud Omar (Cercle Brugge, Ubelgiji), Philemon Otieno (Gor Mahia), Jockins Atudo (Posta Rangers), Dennis Odhiambo (Sofapaka), Joash Onyango (Gor Mahia), Benard Ochieng (Vihiga United);

Viungo – Victor Wanyama (Tottenham Hotspurs, Uingereza), McDonald Mariga (Real Oviedo, Uhispania), Clifton Miheso (Buildcon FC, Zambia), Paul Were (FC Kaisar, Kazakhstan), Ismael Gonzales (CF Fuenlabrada, Uhispania), Eric Johanna (IF Brommapojkarna, Uswidi), Johanna Omollo (Cercle Brugge, Ubelgiji), Anthony Akumu (Zesco, Zambia), Whyvonne Isuza (AFC Leopards), Francis Kahata (Gor Mahia), George Odhiambo (Gor Mahia), Duncan Otieno (AFC Leopards), Samuel Onyango (Gor Mahia);

Washambuliaji – Michael Olunga (Kashiwa Reysol, Japan), Ovella Ochieng (Vasalund, Uswidi), Jesse Were (Zesco, Zambia), Masud Juma (hana klabu), Cliff Nyakeya (Mathare United), Abdallah Hassan (Bandari), Piston Mutamba (Sofapaka) na Allan Wanga (Kakamega Homeboyz).

Ghana

Makipa – Lawrence Ati (Sochaux, Ufaransa), Richard Ofori (Martizburg, Afrika Kusini);

Mabeki – Harrison Afful (Columbus, Marekani) Daniel Opare  (Antwerp, Ubelgiji), Kassim Nuhu (1899 Hoffenheim, Ujerumani), John Boye (FC Metz, Ufaransa), Daniel Amartey ( Leicester City, Uingereza), Andy Yiadom (Reading, Uingereza), Nicholas Opoku (Udinese, Italia);

Viungo – Afriyie Acquah (Empoli, Italia), Isaac Sackey (Alanyaspor, Uturuki), Ebenezer Ofori (New York City FC, Marekani), Christian Atsu (Newcastle, Uingereza), Edwin Gyasi (CSKA Sofia, Bulgaria), Kwadwo Asamoah (Inter Milan, Italia), Frank Acheampong (Tianjin Teda, Uchina), Nana Ampomah (Waasland-Beveren, Ubelgiji);

Washambuliaji – Raphael Dwamena (Levante, Uhispania), Thomas Partey (Atletico Madrid, Uhispania), Majeed Waris (Nantes) na William Owusu (Antwerp, Ubelgiji).