Boca Juniors wanyanyua taji la kwanza la Diego Maradona Cup

Boca Juniors wanyanyua taji la kwanza la Diego Maradona Cup

Na MASHIRIKA

BOCA Juniors walitwaa taji la Diego Armando Maradona Cup mnamo Januari 17 baada ya kuwapiga Banfield 5-3 kupitia mikwaju ya penalti.

Maradona aliagana dunia mnamo Novemba 2020 na Argentina ikabadilisha jina la kipute chao cha League Cup kwa heshima za jagina huyo wa soka aliyewahi kuvalia jezi za Boca.

Boca walijiweka uongozini kupitia Edwin Carmona lakini Luciano Lollo akasawazisha mambo kwa upande wa Banfield mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Bao hilo la Banfield lilipachikwa wavuni sekunde chache baada ya Emmanuel Mas wa Boca kuonyeshwa kadi nyekundu.

Boca walifunga mikwaju yao yote mitano ya penalti huku Jorge Rodriguez akipoteza penalti yake kwa upande wa Banfield.

“Taji hili ni kwa heshima za marehemu Maradona aliyekuwa nguli wa soka kambini mwetu. Tuna hakika yuko nasi katika sherehe zetu za kufurahia ufanisi huu,” akasema mshambuliaji Ramon Abila wa Boca.

Boca wanatwaa taji la Maradon Cup  siku chache baada ya kubanduliwa na Santos kwenye kampeni za kuwania ufalme wa Copa Libertadores msimu huu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

ReplyForward
  • Tags

You can share this post!

Lewandowski aweka rekodi mpya ya ufungaji Bundesliga

Kioja waumini wakivunja makufuli sita kanisani