NA KNA
Polisi katika Kaunti ya Mombasa wameonya wahudumu wa bodaboda dhidi ya kujihusisha na ghasia wakati wa kampeni za kisiasa.
Kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Mvita, Bw Joseph Ongaya, alishauri viongozi wa makundi ya bodaboda kuhakikisha wanachama wao hawavunji sheria kwani wakifanya hivyo wataadhibiwa kama wahalifu wengine.
Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa viongozi wapya wa wahudumu hao Tononoka, Bw Ongaya pia aliwatahadharisha dhidi ya kuingia barabarani bila leseni.