Bodaboda kutoka Kenya wafurika Uganda kwa mafuta

Bodaboda kutoka Kenya wafurika Uganda kwa mafuta

Brian Ojamaa na Titus Ominde

WAENDESHAJI bodaboda na wahudumu wa matatu katika Kaunti ya Busia wamegeukia kununua mafuta kwa bei nafuu Uganda baada ya serikali kuongeza bei ya bidhaa hiyo nchini.

Wamekosoa vikali hatua hiyo wakisema imejiri wakati wanajaribu kupata afueni kutokana na athari za Covid-19.Wahudumu hao wanaoendesha shughuli zao kwenye mpaka wa Busia na Malaba, walikimbilia kupata afueni katika taifa hilo jirani kufuatia tangazo la Mamlaka ya Kawi na Petroli (EPRA) la kupandisha bei ya mafuta.

“Tunapata hasara kwa sababu wateja wetu wanaamua kutembea ili kuepuka kulipia zaidi ya wanavyoweza kumudu,” akasema Bw David Oguna.

Wakati huo huo, mwinjilisti na mwimbaji anayepania kuwania kiti cha urais mwaka wa 2022, Reuben Kigame amewakosoa wabunge kutokana na mfumuko wa bei ya mafuta cnhini.

Akizungumza mjini Eldoret, Bw Kigame alisema hatua ya wabunge kuunga mkono sheria ya kuongeza ushuru wa bidhaa muhimu ndiyo chanzo cha ongezeko hilo la bei.

 

You can share this post!

Kanuni mpya kwa walimu wa nyanjani

Korti sasa kuamua hatima ya kesi kuhusu CBC