Bodaboda walia polisi jijini bado wanawadhulumu

Bodaboda walia polisi jijini bado wanawadhulumu

NA JOSEPH NDUNDA

MSAKO unaoendelea kuwaondoa wahudumu wa bodaboda katikati ya jiji la Nairobi unasemekana kugeuzwa kuwa kitega uchumi kwa maafisa wa polisi.

Inadaiwa kuwa maafisa wa polisi wanawaitisha wahudumu hao kati ya Sh10,000 na Sh15, 0000 ili kurejeshewa pikipiki zao.

Wiki jana, Rais Uhuru Kenyatta alisitisha msako huo wa kuwanasa wanabodaboda wasiotii sheria kufuatia kisa ambapo mwanamke mmoja alidhulumiwa na kundi la wahudumu hao katika barabara ya Profesa Wangari Maathai.

Lakini sasa wahudumu wa bodaboda wanalalamika kuwa wengi wao walimakatwa bila kosa na pikipiki zao kutwaliwa.

Wanasema hata baada ya serikali kusitisha msako huo, wengi wao bado wanahangaishwa kwa kukamatwa na kulazimishwa kutoa hongo.

Jana Jumatatu, polisi waliendelea kuwakamata wahudumu hao katikati mwa jiji la Nairobi, wakidai wafanyabiashara hao hawana stakabadhi hitajika.

Baadhi ya mahitaji ambayo wahudumu hao wanatakiwa kuwa nayo ni leseni za uendeshaji, bima, kofia na jaketi miongoni mwa mahitaji mengine.

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Hofu ya ongezeko la visa vya ukoma nchini

Owino: Hatuendi kutalii Ghana bali kushindana

T L