Bodi kuchunguza wanaouza dawa bila ushauri wa daktari

Bodi kuchunguza wanaouza dawa bila ushauri wa daktari

NA WANGU KANURI

BODI ya Dawa na Sumu (PPB), imeraiwa kuchunguza kliniki na maduka yanayouza dawa, kubaini yanayouza dawa ya ketamine bila ushauri wa daktari katika Kaunti ya Laikipia.

Kamishna wa kaunti hiyo, Joseph Kanyiri, alisema kuwa kumeripotiwa ongezeko la matumizi mabaya ya dawa hiyo ambayo hutumika sana kwa matibabu ya wagonjwa wa akili.

“Dawa hiyo ya ketamine ambayo mitaani inajulikana kama kete inanunuliwa kwa wingi na watu ambao wanaiuza kwa watoto na kuwaathiri akili,” Kanyiri anasema.

Dawa hiyo baada ya kununuliwa, huchanganywa na petroli kidogo na bangi na huathiri mwili inapovutwa.

“Tumewaona watoto wadogo wakiathirika kutokana na dawa hii pamoja na zingine kama cocaine. Tunawarai wazazi kuwajibika katika malezi kwa kujua watoto wao wanashirikiana na akina nani wanapotoka nyumbani,” anaongeza.

Kwa mujibu wa kaunti, kamishina huyo, vijana kadhaa wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kuuza dawa za kulevya.Katika maeneo kama Nyahururu, Bw Kanyiri anasema kuwa wamewatia mbaroni wafanyikazi katika baa zinazouza pombe kali.

  • Tags

You can share this post!

Raila atangaza makabiliano

TIBA NA TABIBU: Wanasayansi watahadharisha kuhusu uraibu wa...

T L