Michezo

Bondia Andiego apigwa breki safari ya Olimpiki

March 7th, 2024 1 min read

Na CHARLES ONGADI

JUHUDI za bondia wa kike Elizabeth Andiego kufuzu kushiriki Michezo ya Olympiki zimepigwa breki kali baada ya kushindwa na Stonkute Gabrielle wa Lithuania kwa wingi wa alama katika Mashindano ya Dunia yanayoendelea nchini Italia.

Andiego anayecheza katika uzani wa Middle, aliwekewa matumaini makubwa na mashabiki wengi nchini.

Lakini matokeo ya Jumatano yaliiacha Kenya na mabondia watatu kati ya sita waliowakilisha taifa katika mashindano hayo.

Majaji wote watano walimpatia ushindi Gabrielle.