Boresha Afya: Kukaza misuli ya mwili

Boresha Afya: Kukaza misuli ya mwili

NA PAULINE ONGAJI

SIKU hizi mabinti wengi wanajikaza kudumisha umbo linalopendeza. Mojawapo ya mbinu wanazotumia ni kuzidisha makalio yao ambapo kunao wanaovalia suruali au sketi za jeans zinazowabana huku nia yao ikiwa ni kuvuta macho ya wapita njia.

Wanaofanya hivi hawajui kwamba kuna mbinu salama na za kawaida zinazohusisha lishe na mazoezi, ambazo zaweza saidia kuimarisha mwonekano wa umbo.

Mbinu hizi ni:

Mazoezi: Kuna baadhi ya mazoezi ambayo yaweza tumika kuthibitisha misuli ya sehemu hii na hivyo kudumisha umbo. Haya ni pamoja na squat, leg lift, side squats, standard lunges na bridges miongoni mwa nyingine nyingi.

Lakini mbinu mwafaka na ambayo haitakutatiza hasa ikiwa unataka kuanza ni:

Lishe bora: Kula vyakula vya protini kwa wingi, hasa zisizo na mafuta mengi. Protini ni muhimu kwa kuunda misuli nyembamba ambayo ni muhimu katika kufanya makalio yako yawe thabiti. Kula vyakula kama vile kuku, samaki, nyama isiyo na mafuta, mayai na bidhaa za maziwa. Mbali na hayo, unashauriwa kula mboga kama vile sukuma wiki, spinachi na broccoli ambazo zina viwango vingi vya protini ya mboga. Pia unashauriwa kula vyakula vya kabohaidreti muhimu mwilini.

Vyakula hivi vinakupa nguvu unayohitaji kwa mwili wako kusalia thabiti. Aidha, jiepushe na vyakula vyenye viwango vingi vya sukari na mafuta. Jiepushe na peremende, vitafunio vya chumvi, vyakula vya haraka kama vile pizza na chipsi miongoni mwa vingine.

Kunywa maji ya kutosha: Kunywa maji glasi moja unapoamka kama mbinu ya kuimarisha mfumo wa umetaboli mwilini. Unashauriwa kunywa kati ya lita mbili na tatu za maji kila siku.

Kudumisha unyevu mwilini huimarisha shughuli za viungo mwilini na kuusaidia kuchoma mafuta mwilini.

  • Tags

You can share this post!

DKT FLO: Harufu mdomoni licha ya kupiga mswaki

SHINA LA UHAI: Upangaji uzazi umeongezeka, lakini elimu...

T L