BORESHA AFYA: Kwa afya ya akili

BORESHA AFYA: Kwa afya ya akili

NA PAULINE ONGAJI

UNAPOPANGA kuzingatia lishe bora, ni jambo la busara kutilia maanani kila sehemu ya mwili wako ikiwa ni pamoja na afya ya akili.

Baadhi ya vyakula ambavyo vikutasaidia ni kama vile;

Samoni: Japo samaki wowote yule ana manufaa kwa ubongo, samoni imethibitishwa kuongoza orodha. Hii ni kwa sababu mbali na kuwa na viwango vya juu vya asidi zilizo na mafuta za omega-3, samaki huyu ana viwango vya juu vya virutubisho vya vitamini D, ambavyo vimehusishwa na viwango vya chini vya msongo wa akili.

Ndege: Ndege kama kuku na bata mzinga huwa na viwango vya juu vya amino acid tryptophan. Kiungo hiki husaidia mwili wako kuzalisha serotonin, kemikali ambayo ni muhimu katika kusaidia ubongo kudhibiti mihemko, kupambana na msongo wa akili na kuimarisha kumbukumbu.

Nafaka ambazo hazijakobolewa: Mbali na kukupa protini na nguvu, nafaka hizi zitasaidia ubongo wako kufyonza asidi ya tryptophan, ambayo ni muhimu hasa kwa ubongo wa mtoto anayekua.

Parachichi: Tunda hili lina viwango vya juu vya virutubisho vya vitamini K na folate, ambavyo husaidia kulinda ubongo wako dhidi ya kiharusi. Parachichi pia zina viwango vya juu vya lutein, kiungo ambacho kimehusishwa na shughuli thabiti za ubongo.

Spinachi: Pamoja na mboga zingine za kijani, spinachi ina viwango vya juu vya folic acid, kiungo ambacho kimethibitishwa kukinzana na msongo wa akili. Pia husaidia kukabiliana na tatizo la kukosa usingizi, shida ambayo imehusishwa na matatizo ya kiakili.

You can share this post!

Kamagiras 20 wakamatwa na polisi katika mtaa wa mabanda wa...

Zogo lazuka kikao cha kutimua gavana

T L