BORESHA AFYA: Vyakula kutuliza uchungu wa hedhi

BORESHA AFYA: Vyakula kutuliza uchungu wa hedhi

NA PAULINE ONGAJI

WAKATI wa hedhi wanawake wengi hukumbwa na matatizo mbali mbali kama vile kuumwa na tumbo, misuli na sehemu ya chini ya mgongo, uchovu, tumbo kuvimba, mabadiliko ya mihemko, kuendesha, kuumwa na kichwa, uchungu kwenye matiti na hata chunusi.

Badala ya kutumia dawa kila mara wakati huu, kuna baadhi ya vyakula ambavyo vitakusaidia kutuliza maumivu. Baadhi ya vyakula hivyo ni:

  • ¬∑Mboga na matunda: Mboga na matunda huwa na viwango vya juu vya nyuzi na hii husaidia hupunguza maumivu yanayotokana na hedhi.
  • Maji: Kunywa maji ya kutosha ni muhimu kwa afya na wakati wa hedhi kwani yaweza punguza uwezekano wa kukumbwa na maumvu ya kichwa yanayotokana na kukaukiwa. Pia hii itakusaidia kukabiliana na tatizo la tumbo kuvimba.
  • Samaki na vyakula vya baharini: Samaki kama vile samoni, tuna, sadini na chaza, zina viwango vya juu vya asidi zilizo na mafuta za omega-3. Virutubisho hivi vyaweza punguza maumivu ya mwili wakati huu.
  • Chokoleti: Mbali na kuwa tamu, chokoleti ina viwango vya juu vya madini ya chuma na magnesium. Kula kiwango cha kutosha cha chokoleti kutakusaidia kukabiliana na upungufu wa madini ya chuma wakati huu. Hedhi husababisha viwango vya chuma kupungua kwani mhusika hupoteza damu, na huenda hali hii ikasababisha anemia kwa wanawake waanaovuja kiwango cha juu cha damu.
  • Pojo na maharagwe: Pojo na maharagwe ni vyakula vilivyo na viwango vya juu vya chuma na protini.

Kula viwango vya juu vya protini wakati wa hedhi husaidia kupunguza hamu ya kula vyakula vingine visivyo vya afya.

Vyakula hivi vina viwango vya juu vya madini ya zinc, ambayo husaidia kupunguza maumivu yanayotokana na hedhi.

Lakini hata unapochagua vyakula vya kula wakati huu, kuna vingine ambavyo huchochea au kuongeza maumivu na hivyo vinapaswa kuepukwa.

Vyakula hivi ni pamoja na vyakula vilivyohifadhiwa na kemikali, vyakula vilivyo na viwango vya juu vya sukari, bidhaa zilizookwa na unga mweupe wa ngano, vyakula vinavyosababisha gesi tumboni kama vile koliflawa.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Ugonjwa wa tezi umeanza kuweka wadau wasiwasi

Wanaume wamo hatarini zaidi kuugua figo – Wataalamu

T L