Kimataifa

Boris Johnson agundulika ana virusi vya corona

March 27th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

LONDON, UINGEREZA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema vipimo vimebainisha ana virusi vya corona; ameweka maelezo katika ukurasa wa akaunti yake ya Twitter.

“Kwa kipindi cha saa 24 nimekuwa na dadili dhaifu za virusi vya corona na vipimo vimebainisha ni kweli ninavyo,” ameandika Johnson.

Kiongozi huyo amesema anajitenga, lakini akaondoa hofu akisema kwamba ataendelea kuiongoza serikali na kusimamia mchakato wa kukabiliana na maradhi ya Covid-19 kupitia makongamano ya video.