Borussia Dortmund wakomoa Leverkusen katika Bundesliga

Borussia Dortmund wakomoa Leverkusen katika Bundesliga

Na MASHIRIKA

BAO la kipindi cha kwanza kutoka kwa Marco Reus lilisaidia Borussia Dortmund kuanza kampeni za Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen.

Leverkusen walikamilisha mchuano huo na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya Lukas Hradecky kuonyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha pili.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Dortmund kusakata ligini bila Erling Haaland aliyeyoyomea Uingereza kuvalia jezi za Manchester City. Sebastien Haller aliyesajiliwa na Dortmund kujaza pengo la Haaland alikosa gozi dhidi ya Leverkusen kwa sababu ya ugonjwa.

Dortmund walikamilisha kampeni za Bundesliga msimu jana katika nafasi ya pili jedwalini kwa alama 69, nane nyuma ya miamba Bayern Munich waliofungua msimu huu kwa ushindi mnono wa 6-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mistari ya mwisho

Brighton waangusha Man-Utd ya kocha Ten Hag katika EPL...

T L