Bournemouth wamtwaa mshambuliaji Morgan Rogers kutoka Man-City

Bournemouth wamtwaa mshambuliaji Morgan Rogers kutoka Man-City

Na MASHIRIKA

BOURNEMOUTH wamejitwalia huduma za fowadi Morgan Rogers kutoka Manchester City kwa mkopo wa mwaka mmoja huku wakiwa huru kumpa sogora huyo mwenye umri wa miaka 19 mkataba wa kudumu mwishoni mwa muhula huu wa 2021-22.

Rogers ambaye ni raia wa Uingereza, alianza kupiga soka ya kulipwa kambini mwa West Bromwich Albion kabla ya kusajiliwa na Man-City mnamo 2019.

Kabla ya kuhamia Bournemouth kwa mkopo, alitia saini mkataba mpya wa hadi 2024 kambini mwa Man-City ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Aliwajibikia kikosi cha Ligi ya Daraja ya Pili nchini Uingereza (League One), Lincoln City kwa mkopo wa miezi sita msimu uliopita wa 2020-21 na akafungia klabu hiyo mabao sita kutokana na mechi 28.

Ingawa Lincoln walitinga hatua ya mchujo wa kufuzu kwa Ligi ya Daraja ya Kwanza (Championship), walizidiwa ujanja na Blackpool waliowadengua.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

NGILA: Serikali isianzishe mradi mpya, ikamilishe Konza

Omondi na klabu yake ya Jonkopings waonja ushindi wa pili...