Brentford yadhalilisha Manchester United katika EPL

Brentford yadhalilisha Manchester United katika EPL

Na MASHIRIKA

BRENTFORD waliendeleza masaibu ya kocha Erik ten Hag na waajiri wake Manchester United mnamo Jumamosi usiku kwa kuwapokeza kichapo cha 4-0 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ugani Gtech Community.

Mabao yote ya Brentford wanaonolewa na kocha Thomas Frank yalifumwa wavuni chini ya dakika 35 za kipindi cha kwanza kupitia Josh Dasilva, Mathias Jensen, Ben Mee na Bryan Mbeumo.

Kichapo hicho ni cha saba mfululizo kwa Man-United kupokezwa ugenini, hiyo ikiwa rekodi mbovu zaidi katika historia ya mabingwa hao mara 20 wa EPL tangu 1936. Aidha, ni mara ya saba kwa Man-United kufungwa mabao manne katika kipute cha EPL tangu mwanzo wa msimu uliopita wa 2021-22.

Huku ushindi wa Brentford ukiwa wa kihistoria, Ten Hag ana kibarua kizito cha kunyanyua kikosi chake kitakachovaana na Liverpool ugani Old Trafford mnamo Agosti 22, 2022. Man-United walianza kampeni za EPL msimu huu kwa kichapo cha 2-1 dhidi ya Brighton mnamo Agosti 7, 2022 ugani Old Trafford.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kioni: UDA ilichezea Jubilee rafu Mlimani

Wagombeaji wa DAP-K walaumu Oparanya kwa kushindwa

T L