Brigid Kosgei ajiondoa London Marathon kuuguza jeraha

Brigid Kosgei ajiondoa London Marathon kuuguza jeraha

Na GEOFFREY ANENE

MSHIKILIZI wa rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 42 ya wanawake Brigid Kosgei amejiondoa kutoka makala ya 42 ya London Marathon yatakayofanyika nchini Uingereza mnamo Oktoba 2.

Bingwa huyo wa London Marathon 2019 na 2020 amechukua hatua hiyo baada ya kushauriana na kocha na timu yake akielekeza kuwa amejiondoa kwa sababu ya jeraha katika mguu wake wa kulia.

“Ni jeraha ndogo, lakini limenisumbua kwa mwezi mmoja. Matayarisho yangu yamekuwa ya kukatizakatiza kwa hivyo si mazuri kwa mashindano makubwa kama London Marathon,” amenukuliwa akisema Jumatatu.

Aliongeza, “Tumeamua ni busara kujiondoa kutoka kwa makala ya mwaka huu na kutafuta matibabu zaidi ili niingie 2023 nikiwa imara kabisa.”

Kosgei anashikilia rekodi ya dunia ya umbali huo ya saa 2:14:04 ambayo aliweka akitwaa taji la Chicago Marathon nchini Amerika mwaka 2019.

Kosgei alishinda Tokyo Marathon mapema mwaka huu akiandikisha 2:16:02.

Wakali Joyciline Jepkosgei (Kenya) na Yalemzerf Yehualaw (Ethiopia) wanasalia katika orodha ya watimkaji wanaopigiwa upatu kutawala mjini London. Jepkosgei anatetea taji.

  • Tags

You can share this post!

Ebola: Idadi ya vifo yaongezeka Uganda

Watu 3 wafariki katika eneo la Kirigiti baada ya jengo la...

T L