Broadways yazindua mkate usio na sukari

Broadways yazindua mkate usio na sukari

Na LAWRENCE ONGARO

KAMPUNI ya mikate ya Broadways mjini Thika, imezindua mkate mpya wa mchanganyiko wa unga aina mbili ambazo ni nyeupe na hudhurungi.

Mkurugenzi wa Broadways Bw Bimal Shah, alisema bidhaa hiyo mpya ni ya kipekee kwa sababu haina sukari yoyote.

“Tumezindua bidhaa mpya kwa lengo la kunufaisha wateja wengi ambao wana matatizo ya kiwango cha sukari mwilini.”

Alisema mkate waliozindua ni bora kwa Afya ya binadamu kwa sababu haina sukari yoyote, inaongeza nguvu mwilini, na pia ina ladha tamu.

Mbali na Wakenya kula mikate, amewahimiza kulinda afya yao kwa kula matunda kwa wingi kama machungwa na maembe.

Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli moja eneo la Kasarani mnamo jumatano, ulihudhuriwa na wafanyi biashara wengi na washika dau kadha.

Alisema baada ya kuwa katika biashara ya kuoka mikate kwa zaidi ya miaka 40 wamezindua bidha hiyo ili kuboresha biashara yao zaidi.

Meneja wa soko Bw Deven Shah, alisema tayari bidhaa hiyo imesambazwa katika duka za jumla kadha nchini.

Alisema mkate waliozindua haina madhara yoyote kwa mwili na ni ya manufaa kubwa kwa wagonjwa wa kisukari.

“Kwa zaidi ya miezi miwili ambayo tumekuwa katika soko wateja wengi wameridhika na bidhaa hiyo huku tukitarajia kusambaa kote nchini,” alisema Bw Shah.

Kando na kampuni hiyo kutoka mikate pia ina kampuni nyingine ya kusaga unga wa ugali na ngano, itwayo Bakex Mill.

Unga unaosagwa katika kampuni hiyo ni Oboma na Phulka floor.

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Tabitha Manzi

BB Erzumspor anayochezea Johanna Omolo yaendelea kufufuka...